Alhamisi, 30 Machi 2023

KISHINDO CHA KAMALA HARRIS TANZANIA!Neema ya Mabilioni Ya Uwekezaji ,SAMIA Aahidi Ushirikiano

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Kikwete Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023.


Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023. Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Machi, 2023. PICHA ZOTE NA IKULU

Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Ikulu Dar es Salaam
Katika hotuba yake Makamu wa Rais wa Marekani alisisitiza wanawake kushiriki katika ukuaji wa uchumi "Wanawake duniani lazima washiriki katika kukuza uchumi, na washiriki kwa usawa hususani kwenye uongozi, ukiinua uchumi wa mwanamke umeinua uchumi wa familia na jamii kwa ujumla

Aliendelea kutoa msisitizo na kusema kuwa "Naamini kwamba kwa mabadiliko na maendeleo yanayoendelea barani Afrika na Tanzania yatatengeneza kesho nzuri ya dunia na yatanufaisha dunia nzima"
Kwa upande wake mwenyeji wake Rais Samia alisema kuwa "Katika sekta ya afya UKIMWI na kifua kikuu havitishii tena maisha ya watu wetu, maambukizi ya UKIMWI yameshuka kutoka asilimia 7.2 mwaka 2012 hadi asilimia 4.7 mwaka 2016/17 na imepungua zaidi mwaka 2021"

Alisisitiza suala la visa kati ya Marekani na Tanzania "Kuna suala la Visa kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa watu na mizigo kati ya nchi zetu mbili, na katika hilo Tanzania inakaribisha utayari wa Marekani kufanya mapitio ya mkataba wa sasa wa visa" alisema Rais Samia katika hotuba yake

0 maoni:

Chapisha Maoni